Watoto nchini Uingereza wahitaji msaada

Imebadilishwa: 5 Septemba, 2012 - Saa 09:01 GMT

Shirika la kimataifa la misaada la Save the Children kwa mara ya kwanza limetoa wito wa misaada kusaidia watoto maskini nchini Uingereza.

Shirika hilo linasema kuzorota kwa uchumi na kupanda kwa gharama ya maisha kumechangia familia nyingi nchini Uingereza kuishi katika umaskini.

Baadhi ya watoto wanakwenda shule wakiwa na njaa na bila mavazi ya msimu wa baridi.

Shirika hilo linataka dola elfu mia nane kusaidia watoto kote nchini Uingereza.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.