Benki ya Ulaya kunusuru uchumi wa Ulaya

Imebadilishwa: 6 Septemba, 2012 - Saa 16:18 GMT

Benki Kuu ya Ulaya imetangaza mipango ya kushughulikia mgogoro wa madeni katika nchi zinazotumia sarafu ya Euro kwa kununua dhamana za serikali za nchi zinazokabiliwa na madeni makubwa katika Muungano huo.

Benki hiyo ina matumaini kwamba itakuwa rahisi kwa nchi kama Hispania na Italia kupata fedha zinazohitajika katika kukwamua uchumi wa nchi hizo.

Rais wa Benki ya Ulaya, ECB Mario Draghi amerejelea ahadi yake ya kufanya kila njia ili kunusuru sarafu ya Euro, huku akieleza kuwa uungaji mkono ununuzi wa dhamana za serikali ukikubaliwa kwa kauli moja.

Bei ya hisa katika masoko ya Ulaya na Marekani zilipanda kufuatia uamuzi huo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.