Mwanamfalme Harry kuhudumu Afghanistan

Imebadilishwa: 7 Septemba, 2012 - Saa 11:32 GMT

Mwanamfalme wa Uingereza Harry ambaye ni wa tatu kwenye orodha ya kuurithi ufalme ameanza ziara yake ya pili ya kikazi katika jeshi la Uingereza huko Afghanistan.

Ataongoza helikopta ya kivita katika mapambano dhidi ya kundi la wapiganaji wa Taliban.

Maafisa waliamua kuwa hatua ya kutangaza hadharani ziara ya Prince Harry nchini Afghanistan, haitamweka katika hatari yoyote mwanamfalme huyo pamoja na wanajeshi wenzake.

Ziara yake ya awali huko Afghanistan ilikatizwa baada ya vyombo vya habari kufichua taarifa hizo kinyume na ilivyokuwa imekubaliwa rasmi kuzibana.

Mwandishi wa BBC huko Kabul anasema hatua hii inaweza kumsaidia Harry ambaye aligonga vichwa vya habari duniani baada ya kuchapishwa kwa picha ambazo alionekana akitembea uchi katika chumba cha hoteli mjini Las Vegas Marekani.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.