Waumini washambuliwa mjini Damascus

Imebadilishwa: 7 Septemba, 2012 - Saa 11:52 GMT

Bomu limelipuka nje ya msikiti mmoja mjini Damascus, watu walipokuwa wanatoka katika maombi ya siku ya Ijumaa.

Kwa mujibu wa taarifa za televisheni ya taifa, watu kadhaa wamejeruhiwa katika shambulizi hilo ambalo imebainika kuwa bomu lililolipuka lilikuwa limetegwa kwenye pikipiki.

Katika tukio lengine, mkuu wa shirika la msalaba mwekundu, Peter Maurer, alisema kuwa ana matumaini kuhusu mazungumzo yake na rais Bashar al-Assad pamoja na maafisa wengine wa serikali ya Syria kuhusu juhudi za kutoa misaada nchini Syria.

Lakini alisema kuwa hatua itaweza tu kupigwa ikiwa serikali itaweza kutekeleza makubaliano waliyoafikia wakati wa ziara yake ya siku tatu.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.