Misri yaua watu 30 Sinai

Imebadilishwa: 8 Septemba, 2012 - Saa 12:44 GMT

Misri inasema kuwa wanajeshi wake wameuwa watu zaidi ya 30, walioelezewa kuwa wahalifu, tangu kuanza operesheni kubwa ya usalama mwezi uliopita, katika ras ya Sinai.


Msemaji wa jeshi la Misri Ahmed Mohammed Ali, amesema operesheni hiyo inafuatia mauaji ya walinzi wa mpakani wa Misri 16, yaliyofanywa na wapiganaji wa Kiislamu. Aliongeza kuwa operesheni hiyo iligundua njia za chini kwa chini 30 baina ya Sinai na Gaza na kusema kuwa njia hizo zimeteketezwa.

Ahmed ameeleza kuwa operesheni hiyo itaendelea hadi lengo lake lifikiwe, akisisitiza pia kuwa hatua hiyo haiendi kinyume na mkataba wa amani na Israel.

Wakuu wa Israel, faraghani walisema walikuwa na wasiwasi kuwa wanajeshi wa Misri wamekusanywa katika eneo la Sinai, eneo ambalo halitakiwi kuwa na harakati za kijeshi, kufuatana na mkataba wa amani baina ya nchi mbili hizo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.