Zimbabwe yalalamikia mauzo ya almasi

Imebadilishwa: 9 Septemba, 2012 - Saa 16:28 GMT

Waziri wa Fedha wa Zimbabwe, Tendai Biti, amesema kuwa amevunjika moyo kuwa wizara yake inapata sehemu ndogo ya kile alichotarajia kutoka mauzo ya almasi.


Zimbabwe ni kati ya nchi zenye madini mengi ya almasi, lakini Bwana Biti anasema nchi yake hainufaiki na utajiri huo.

Akizungumza na waandishi wa habari, alisema katika mauzo ya almasi ya tangu mwaka huu kuanza, ya thamani ya karibu dola nusu bilioni, wizara ya fedha imepata chini ya asilimia 10 tu ya pato hilo.

"Vipi inakuaje mauzo ya dola laki nne na elfu hamsini na sita ya almasi, yanamudu kulipa dola milioni 41 kwa mwaka mzima?
Na mmi sifikiri kama ni suala la wizara ya fedha tu peke yake.
Watumishi wa serikali wanataka baha-shishi, wanataka nyongeza ya mishahara." Alisema.

Baadhi ya makampuni ya migodi yanasema, Bwana Biti alikisia vibaya mauzo ya almasi kwenye majeti yake ya mwaka huu, na sasa anajaribu kuyalaumu makampuni kwa makosa yake mwenyewe.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.