Safari za mwisho za Air Nigeria

Imebadilishwa: 10 Septemba, 2012 - Saa 13:51 GMT

Shirika la kitaifa la ndege nchini Nigeria, Air Nigeria, linafanya safari zake za mwisho leo baada ya kusitisha shughuli zake kimataifa na kuwaachisha kazi takriban wafanyakazi mianane.

Waekezaji wa shirika hilo, wamekuwa na wakati mgumu kulipa madeni yake ya hadi dola bilioni laki mbili na nusu walizotumia kununua shirika hilo kutoka kwa kampuni ya ndege ya uingereza, Virgin, miaka miwili iliyopita.

Hatua ya kufungwa kwa shirika hilo, iniacha nchi hiyo na mashirika manne tu ya ndege ambayo yanafanya tu safari kwa mpangilio, hatua ambayo inadumaza uchumi.

Wiki jana halmashairi ya safari za ndege za kimataifa, IATA, ilisema kuwa tatizo kubwa zaidi kwa mashirika ya ndege barani Afrika ni usalama. Rekodi ya ajali za ndege barani Afrika ni mbaya zaidi ikilinganishwa na ile ya kimataifa.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.