Wanademokrasia washinda uchaguzi Hong Kong

Imebadilishwa: 10 Septemba, 2012 - Saa 12:08 GMT


Wakereketwa wa demokrasia huko Hong kong wameshinda zaidi ya thuluthi moja ya viti katika bunge la nchi hiyo.

Viti hivyo vinatosha kupiga kura ya turufu dhidi ya jaribio lolote za kuzuia raia wote kushiriki katika upigaji kura kwenye uchaguzi ujao.

Walitoshana viti na vyama vinavyounga mkono Beijing lakini wakashindwa kwenye viti vilivyotengewa makundi maalum.

Wanaharakati wanasema kuwa wakereketwa hao wa demokrasia walishindwa kutumia fursa iliyotokana na maandamano ya majuma kadhaa yaliyoshurutisha serikali kufutilia mbali mpango wa kuanzisha somo la uzalendo wa China katika shule za Hongkong.

Kiongozi wa chama kikuu cha demokrasia Albert Ho, alijiuzulu akilaumu mgawanyiko katika chama kwa matokeo hayo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.