Mpango mpya kukwamua uchumi Ufaransa

Imebadilishwa: 10 Septemba, 2012 - Saa 08:49 GMT

Rais wa Ufaransa , Francois Hollande, ametangaza mpango wa miaka miwili wa kukwamua uchumi wa nchi hiyo unaoyumba.

Alikuwa akiongea katika mahojiano yaliyolenga kujibu ukosoaji wa namna anavyoshughulikia taasisi za taifa za kifedha na kushuka kwa uungaji mkono dhidi yake katika kura ya maoni.

Bwana Hollande amesema serikali yake imepunguza kiwango cha malengo yake ya ustawi kwa mwaka ujao , ikibana matumizi na kuongeza kodi, huku kundi jipya litakalonufaika likiwa ni asilimia 75 ya watu wanaolipwa zaidi ya euro milioni kwa mwaka .

Pia ameahidi kumaliza ongezeko la idadi ya watu wasio na ajira katika muda wa miezi kumi na miwili

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.