Wito wa usimamizi wa benki Ulaya

Imebadilishwa: 12 Septemba, 2012 - Saa 10:39 GMT

Rais wa tume ya Ulaya, Jose Manuel Barroso, ametaka kuwepo kwa mbinu moja maalum ya kusimamia benki elfu sita katika kanda ya Ulaya.

Katika hotuba yake ya kila mwaka kwa bunge, Bwana Barroso amesema kuwa matatizo ya kiuchumi ya Muungano wa Ulaya yanachangia msimamo wa kutafuta umaarufu bila kujali wananchi Ulaya.

Alisistiza kuwa kuna haja ya kuungana zaidi huku Jumuiya ya Ulaya inapojipanga kuwa shirikisho la mataifa wanachama.

Mwandishi wa BBC anasema kuwa mapendekezo ya kuifanyia marekebisho sekta ya benki ambayo yanaipa uwezo mkubwa benki kuu ya Ulaya, ni hatua muhimu ya kwanza ya kuimarisha muungano katika eneo la Ulaya.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.