240 wafariki katika mkasa wa moto Pakistan

Imebadilishwa: 12 Septemba, 2012 - Saa 15:19 GMT

Zaidi ya watu mia mbili arobaini wamefariki dunia katika mkasa mkubwa wa moto uliotokea katika kiwanda cha kutengeneza nguo katika mji mkubwa zaidi nchini Pakistan, Karachi.

Mamia kadhaa ya watu waliruka kutoka paa la jengo hilo wakijaribu kujiokoa lakini wengi wakiwemo wanawake na watoto walinaswa katika jengo hilo lenye orofa nyingi.

Karibu magari arobaini ya wazima moto yalipambana na moto huo usiku kucha.

Walioshuhudia moto huo mkubwa, walielezea kuona watu wakining'inia katika madirisha ya ghorofa za juu na kisha kuruka chini wakijaribu kujiokoa.

Afisaa mmoja mkuu nchini humo alisema kuwa madirisha yalikuwa yamefungwa kwa vyuma na kiwanda hicho hakikuwa na vyumba salama vya kutorokea wakati moto ukizuka.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.