Wapenzi wa jinsia moja wauawa Iraq

Imebadilishwa: 12 Septemba, 2012 - Saa 11:10 GMT

Uchunguzi wa BBC umebaini kuwa polisi nchini Iraq wanahusika katika mauaji yaliyopangwa ya wapenzi wa jinsia moja .

Wanaharakati wanasema mamia ya wapenzi wa jinsia moja wakiume na baadhi ya wakike, waliuawa katika mauaji ya kulengwa katika miaka ya hivi karibuni, na serikali imefumbia macho mauaji hayo.

Msemaji wa serikali ya Iraq amekanusha kuwepo kwa tatizo lolote.

Amesema kama kuna maafisa wa polisi waliokiuka haki za binadamu walifanya hivyo kama watu binafsi .

Umoja wa Mataifa umethibitisha kuwa unahofu juu ya kampeni ya kikatili dhidi ya wapenzi wa jinsia moja nchini Iraq.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.