Kampuni ya madini ya Platinum yafungwa

Imebadilishwa: 13 Septemba, 2012 - Saa 09:25 GMT

Kampuni kubwa duniani ya uzalishaji wa madini ya Platinum imefunga shughuli zake kuu nchini Afrika kusini, ili kulinda usalama wa wafanyakazi wake .

Kampuni hiyo imesema wafanyakazi wake wanakabiliwa na vitisho kutoka kwa mamia ya wachimba migodi waliogoma, ambao wamefunga barabara karibu na kiwanda chake cha Rustenburg .

Hali ya wasi wasi imetanda katika sekta ya madini kote nchini Afrika kusini baada ya mgomo wa mwezi uliopita katika mgodi wa Marikana kusababisha ghasia ambapo watu zaidi ya arobaini waliuawa.

Mwanasiasa mwenye utata wa Afrika kusini , Julius Malema, aliwahutubia wachimba migodi jumanne , akiwatolea wito kuwafuta kazi viongozi wao ambao aliwashutumu kutotekeleza wajibu wao.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.