Mpinzani wa rais Putin afukuzwa bungeni

Imebadilishwa: 14 Septemba, 2012 - Saa 12:08 GMT

Nchini Urusi, mmoja wa wapinzani wakubwa wa rais Vladmir Putin na kiongozi wa maandamano ya hivi maajuzi ya wafuasi wa upinzani, Gennady Gudkov, amefukuzwa bungeni.

Katika kura ya kwanza ya aina yake katika kipindi cha miaka kumi na saba, wanasiasa wa bunge la waakilishi linalofahamika kama DUMA, walionyesha kwa idadi kubwa kuunga mkono hatua ya kutimuliwa kwa bwana Gudkov, kutokana na kile wanachozingatia kuwa kujihusisha na biashara mbali mbali zinazohitalifiana na maadili.

Kutimuliwa kwake kuna maana kuwa amepoteza ulinzi wa sheria dhidi ya kushtakiwa.

Wafuasi wake wanasema hatua hiyo ilichochewa kisiasa.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.