Serikali kupambana na wachimba migodi

Imebadilishwa: 14 Septemba, 2012 - Saa 12:56 GMT

Serikali ya Afrika Kusini imesema kuwa haita stahamili kile ilichoita mikutano haramu wakati ikijaribu kumaliza migomo inayoendelea kusambaa nchini humo na kuathiri sekta ya madini.

Waziri wa sheria Jeff Radebe, amesema kuwa serikali itakabiliana vilivyo na hatua ya wachimba migodi hao kubeba silaha pamoja na kutoa vitisho vya kuzua ghasia.

Alikanusha kuwa sheria ya hali ya hatari huenda ikatumika kama hatua ya serikali kukabiliana na migomo hiyo.

Tangazo la serikali limetolewa baada ya wachimba migodi kukataa pendekezo la kampuni ya Lonmin ya kiwango cha mishahara ambacho inaweza kuwaongeza wachimba migodi hao.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.