Rais Hamid Karzai alaani mauaji

Imebadilishwa: 17 Septemba, 2012 - Saa 07:26 GMT

Rais Hamid Karzai wa Afghanistan amelaani vikali mauaji ya wanawake wanane katika shambulio la angani lililotekelezwa na shirika la kujihami la nchi za Magharibi NATO.

Taarifa ya Bwana Karzai ilikuwa kali. Alishutumu mauaji ya wanawake hao wanane yaliyotekelezwa na wanajeshi wanaoongozwa na Serikali katika mkoa wa Laghman, ambako wanajeshi wa NATO wapo.

Aliongezea kuwa ameteua kamati maalumu ya kuchunguza tukio hilo lililotendeka ili kuthibitisha kilichotokea.

Viongozi wa mkoa wanasema wanawake hao waliuawa walipokuwa wakikusanya kuni katika misitu eneo la milimani.

Msemaji wa vikosi vinavyoongozwa na NATO alituma risala zake za rambirambi. Ndege hiyo ya kijeshi ilikuwa imewalenga wapiganaji lakini huenda iliwaua raia kimakosa.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.