Makampuni ya Japan yafungwa China

Imebadilishwa: 17 Septemba, 2012 - Saa 12:22 GMT

Makampuni kadhaa ya Japan yamesitisha shughuli zao nchini China baada ya siku kadhaa za maandamano dhidi ya Japan kuhusiana na mzozo wa umiliki wa kisiwa wanachozozania.

Kampuni za Panasonic na Canon zimefunga viwanda vyao baada ya kuporwa huku wafanyabiashara wengine wa Japan wakishambuliwa wakati wa maandamano.

Gazeti la chama rasmi cha kikomunisti, The Peoples' Daily, limeonya kuwa Japan huenda ikaathirika kibiashara ikiwa itaendelea na kile kilichotajwa kuwa uchokozi wake kuhusiana na kisiwa hicho kilicho Mashariki mwa China.

Japan imeonya wananchi wake dhidi ya kufanya maandamano siku ya Jumanne , ambayo itakuwa siku ya maadhimisho ya utawala wa Japan Kaskazini Mashariki mwa China mnamo miaka ya thelathini.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.