Maandamano zaidi kupinga filamu Pakistan

Imebadilishwa: 17 Septemba, 2012 - Saa 14:40 GMT


Mtu mmoja Kaskazini Magharibi mwa Pakistan ameuwawa kwa kupigwa risasi katika tukio la hivi punde kwenye maandamano yanayoendelea kuhusiana na filamu iliyoundwa Marekani na ambayo inadhalilisha dini ya kiislamu.

Mamia ya waandamanaji katika eneo la DIR waliteketeza majumba kadhaa yakiwemo hata ya serikali na kufyatuliana risasi na polisi.

Na katika mji mkuu wa Afghanistan Kaabul, umati wa karibu waandamanaji alfu moja umezua rabsha na kuteketeza magari mbali na kuwafyatulia risasi polisi.

Takriban polisi arobaini wamejeruhiwa kwa mawe.

Nchini Lebanoon, Kiongozi wa Hezbollah, Sheikh Hassan Nasrallah, alitoa wito kufanyika kwa maandamano ya wiki nzima, sio tu katika balozi za Marekani bali pia kuzishinikiza serikali za kiislamu kuelezea ghadabu dhidi ya Marekani.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.