Ashtakiwa kwa kukosoa serikali Burma

Imebadilishwa: 20 Septemba, 2012 - Saa 13:54 GMT

Mchapishaji na mhariri wa gazeti moja binafsi nchini Burma amefunguliwa mashitaka ya kuidhalilisha serikali baada ya kuchapisha habari zinazofichua tuhuma za rushwa katika serikali ya nchi hiyo.

Wizara ya madini ya Burma imechukua hatua hiyo baada ya gazeti hilo la The Voice Weekly kuandika shutuma za ukiukwaji katika masuala ya taratibu za fedha mapema mwaka huu.

Hivi karibuni serikali ya kijeshi ya nchi hiyo imekuwa ikijaribu kulegeza vikwazo vya vyombo vya habari ambavyo vinaonekana kuwa ni miongoni mwa vyombo vya habari vinavyokandamizwa sana duniani.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.