Helikopta ya Syria yaanguka Damascus

Imebadilishwa: 20 Septemba, 2012 - Saa 12:55 GMT

Televisheni ya taifa nchini Syria imeripoti kuanguka kwa helikopta ya kijeshi karibu na mji mkuu Damascus baada ya kugongana kidogo na ndege ya abiria ambayo iliweza kutua salama.

Inaarifiwa kuwa ndege ya abiria ilikuwa imewabeba watu miambili.

Taarifa hiyo inasema ndege ya abiria ilitua salama katika uwanja wa ndege wa Damascus.

Mapema, duru za upinzani zilidai kuwa waasi ndio waliidungua helikopta hiyo.

Serikali imekuwa ikitumia helikopta na ndege nyinginezo katika harakati zake dhidi ya waasi.

Mwezi jana wapiganaji wa upinzani walidai kuidungua helikopta nyingine ya serikali.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.