Makabiliano mpakani mwa Israel na Misri

Imebadilishwa: 21 Septemba, 2012 - Saa 15:09 GMT

Mwanajeshi wa Israel na wapiganaji watatu wameuwawa kwenye mapigano mpakani baina ya Israil na Misri.

Israel inasema wapiganaji walikuwa na silaha tele, na walifyatua risasi dhidi ya wanajeshi waliokuwa wakilinda wajenzi wanaorefusha uzio kwenye mpaka wa Israel.

Inaarifiwa kuwa mpiganaji mmoja alirusha bomu.Kuna taarifa kuwa wanajeshi wengine kadhaa wa Israil walijeruhiwa.

Hivi karibuni, jeshi la Misri lilifanya operesheni kubwa dhidi ya wapiganaji wa kiislamu upande wa mpaka wa Misri, baada ya shambulio Kaskazini mwa eneo la Sinai, ambapo wanajeshi 16 wa Misri waliuwawa.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.