Mageuzi ya kiuchumi Korea Kaskazini

Imebadilishwa: 24 Septemba, 2012 - Saa 11:26 GMT

Ripoti kutoka Korea kaskazini zinasema kuwa mageuzi ya kiuchumi yatakayoruhusu wakulima kuweka mazao yao na kushinikiza masoko huru, yanaidhinishwa .

Hatua hiyo inaonekana kulenga kuongeza mazao katika nchi hiyo iliyo na uchumi unaoendeshwa na serikali na unaokumbwa na ukosefu mkubwa wa chakula.

Shirika la habari la Associated Press linaripoti kwamba wakulima tayari wameambiwa kuwa watawasilisha asilimia ndogo ya mazao yao kwa serikali.

Hakuna tangazo rasmi lililotolewa lakini wachambuzi wanaiona kuwa ishara ya uwezekano wa mabadiliko ya mwelekeo chini ya kiongozi mkuu mpya Kim Jong-un.

Masoko huru yamekuweko kwa miaka kadhaa Korea kaskazini lakini hadhi yao haijulikani na hukabiliwa na misako ya serikali isiyofanyika mara kwa mara.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.