Wapiganaji 14 kunyongwa Misri

Imebadilishwa: 24 Septemba, 2012 - Saa 12:31 GMT

Maafisa nchini Misri wamesema kuwa mahakama moja nchini humo imewahukumu kifo wanamgambo 14 kwa mashambulio dhidi ya jeshi na polisi katika rasi ya Sinai mwaka uliopita.

Mahakama ya Ismailia imewahukumu wanamgambo wengine wanne kifungo cha maisha. Wanaume wote ni wafuasi wa kundi la Tawheed na Jihad.

Ripoti zinasema kuwa hukumu ya kifo kwa wanane kati ya 14 hao ilitolewa wakati wahusika hawakuwepo mahakamani.

Polisi mmoja, mwanajeshi mmoja na raia mmoja waliuawa katika mashambulio hayo katika eneo la al Arish mwaka uliopita.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.