Kero la Malkia kuhusu mhubiri Abu Hamza

Imebadilishwa: 25 Septemba, 2012 - Saa 10:58 GMT


Imebainika kuwa Malkia Elizabeth wa Uingereza, alielezea wasiwasi wake kuhusiana na Mhubiri wa Kiislamu mwenye siasa kali, Abu Hamza, kabla ya kutiwa nguvuni na kushtakiwa kwa kutoa matamshi ya chuki mwaka 2006.

Malkia ananukuliwa akielezea kughadhabika kwake kwa kukosekana njia za kumtia nguvuni Mhubiri huyo.

Kwa kawaida, Malkia aliyeshauriana na Waziri wa mambo ya ndani kuhusiana na suala hili, hajihusishi na Siasa wala kuingilia masuala ya kikatiba.

Matamshi ya Malkia yametolewa baada ya Mahakama ya Haki za Binadamu ya Bara Ulaya kukatalia mbali rufaa ya mwisho ya Abu Hamza akipinga kuhamishwa kutoka Uingereza hadi Marekani.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.