Askofu mpya wa kianglikana kuteuliwa

Imebadilishwa: 26 Septemba, 2012 - Saa 14:18 GMT

Jopo la wanachama wakuu wa kanisa la Kianglikana wanakutana leo kumchagua askofu mkuu mpya wa Canterbury kuongoza kanisa hilo.

Wadadisi wanasema kuwa kawaida huwa kuna idadi kubwa ya wagombea wanaoweza kuchukua nafasi ya Askofu mkuu anayestaafu Rowan Williams hali inayoifanya vigumu kujua nani atakayechukua wadhifa wenyewe.

Askofu mpya atachukua uongozi wakati kanisa hilo linakumbwa na migawanyiko kuhusu maswala kadhaa mfano, ikiwa askofu anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja anaweza kutawazwa kama askofu pamoja na kudidimia kwa idadi ya wafuasi wa kanisa hilo kila kukicha.

Jopo hilo litakutana kwa siku tatu kabla ya kuwasilisha jina la askofu mpya.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.