Wakimbizi wavunjiwa kambi Sri Lanka

Imebadilishwa: 27 Septemba, 2012 - Saa 17:15 GMT

Zaidi ya familia miamoja za Tamil nchini Sri Lanka, zinasema kuwa zimefukuzwa kutoka katika kambi za wakimbizi wa ndani na kupelekwa msituni.

Wanasema kuwa jeshi lilivunja kambi zao siku ya Jumanne na kisha kuzifunga.

Familia hizo zinasema kuwa hazijaruhusiwa kurejea nyumbani kwao na zilipewa turuba kujengea hifadhi zingine za muda ambazo baadaye ziliharibiwa na upepo mkali na mvua.

Kambi hizo zilikuwa hifadhi kwa watu walioachwa bila makao baada ya harakati za serikali dhidi ya waasi wa Tamil Kaskazini mwa nchi.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.