Uhispania kujikwamua kiuchumi

Imebadilishwa: 27 Septemba, 2012 - Saa 16:30 GMT

Serikali ya Uhispania inawasilisha bajeti yake leo ambapo itazidi kupunguza mahitaji yake ya mikopo na kujaribu kusawazisha mzigo wake wa ongezeko la deni.

Kuna hisia katika Masoko ya hisa kama Uhispania inaweza kuomba msaada wa nchi za Muungano wa Ulaya kuiondolea mzigo wa kifedha.

Masoko ya fedha duniani yalianza kuonyesha wasiwasi juu ya hali nchini humo wiki hii.

Baraza la serikali limezindua maelezo ya mpango wa kupunguza matumizi ya mamilioni ya euro katika kupunguza matumizi ya pesa na pia kuweka akiba.

Lakini waziri mkuu wa nchi hiyo , Soraya Saenz de Santamaria aliambia mkutano wa waandishi wa habari, kuwa malipo ya uzeeni yataongezwa , serikali itatumia pesa kutoka kwa hifadhi yake na jopo maalum litaundwa kudhibiti matumizi ya pesa za serikali.

Alielezea kuwa zaidi ya mapendekezo arobaini ya mageuzi ya sheria yalilenga kuongeza nafasi za kazi na ushindani.

Wahispania ambao wanakumbwa na mdororo wa uchumi na viwango vya juu vya ukosefu wa ajira, wamekuwa wakijiandaa kwa mipango zaidi ya kupunguza matumizi ya pesa za umma, kupandishwa kwa kodi na mageuzi ya kujaribu kuokoa dola bilioni hamsini za ziada

Serikali imesema kuwa idara zote za serikali lazima zijitolee katika mageuzi haya yote.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.