19 wafariki kwenye ajali ya ndege Nepal

Imebadilishwa: 28 Septemba, 2012 - Saa 09:42 GMT

Watu 19 wameuawa katika ajali ya ndege iliyotokea viungani mwa mji mkuu wa Nepal, Kathmandu.

Msemaji wa polisi, (Binod Singh) amesema kuwa ndege hiyo ndogo iliyomilikiwa na kampuni ya ndege ya Sita Air, ilianza kuteketea dakika mbili baada ya kupaa angani kutoka uwanja wa ndege wa Kathmandu.

Ndege hiyo ilikuwa inasafiri kuelekea eneo la Lukla karibu na mlima Everest. Shughuli za uokozi zinaendelea.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.