Iran yatishia kulipiza kisasi

Imebadilishwa: 28 Septemba, 2012 - Saa 09:19 GMT

Iran imeapa kulipiza kisasi dhidi ya mashambulio yoyote, baada ya wazir mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kutaka wazuiwe kutengeneza sila za kinuklia.

Akihutubia mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa, Netanyahu alionya kuwa hadi pale Iran itakapozuiwa - huenda wakawa na virutubisho vya kutosha vya uranium kutengeneza bomu lake la kwanza la nuklia mwaka ujao.

Alisema ana imani kuwa Marekani na Israel zinaweza kupata njia ya kuzuia mpango huo wa Iran, lakini akasema muda unayoyoma.

Naibu balozi wa Iran katika umoja wa Mataifa Eshagh al-Habib amesema Netanyahu alikuwa akileta madai yasiyo na msingi, na kusema kuwa nchi yake ina nguvu imara ya kujitetea.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.