Jela lavamiwa nchini Iraq, 12 wakiuawa

Imebadilishwa: 28 Septemba, 2012 - Saa 09:50 GMT

Wapiganaji waliojihami kwa Bunduki walivamia Gereza moja katika mji wa Tikrit nchini Iraq na kuwauwa askari jela kumi na wawili kabla ya kutorosha idadi isiyojulikana ya wafungwa.

Afisa mmoja alithibitisha kuwa Maafisa hao wa Polisi waliuawa katika gereza la Tasfirat lililovamiwa na wapiganaji hao na kusema hali imedhibitiwa kwa hivi sasa na maafisa wa usalama.

Shambulizi hilo lililoanza kwa mlipuko wa bomu lilotegwa kwenye gari nje ya lango kuu, lilitekelezwa usiku kucha hadi alfajiri ya ijumaa.

Gereza hilo linawahifadhi mamia ya wafungwa wakiwemo wale wanaoshukiwa kuwa na uhusiano na kundi la Al-Qaeda.

Sheria ya kutotoka nje imetangazwa katika mji wa Tikrit kufuatia uvamizi huo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.