Majeshi ya AMISOM kukomboa Kismayo

Imebadilishwa: 1 Oktoba, 2012 - Saa 12:16 GMT

Taarifa kutoka nchini Somalia, zinasema kuwa wanajeshi wa serikali wameingia katikati mwa mji wa bandarini wa Kismayo siku chache baada ya mji huo kukimbiwa na wapiganaji wa Al Shabaab.

Msemaji wa jeshi la Somalia, ameelezea kuwa mamia ya wanajeshi walihusika katika operesheni hiyo huku majeshi ya AMISOM yakijiandaa kwa mapambano ya kuutwaa mji huo kutoka mikononi mwa Al Shabaab.

Wenyeji wa Kismayo wanasema kuwa wanajeshi wa Kenya waliingia mjini humo kutoka upande wa Magharibi na sasa wanajiandaa kwa makabiliano ya kuukomboa mji wenyewe.

Kismayo ndiyo ilikuwa ngome ya mwisho ya Al Shabaab.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.