Thamani ya Rial Iran yashuka

Imebadilishwa: 1 Oktoba, 2012 - Saa 13:29 GMT

Thamani ya sarafu ya Iran imeshuka kwa kiwango kikubwa dhidi ya Dola ya Marekani licha ya juhudi za serikali kuizuia kuzorota.

Rial ya Iran ilishuka kwa asilimia saba na sarafu hiyo inasemekana imeendelea kuzorota katika siku za hivi karibuni.

Mojawapo ya sababu za kushuka kwa thamani hiyo, ni vikwazo vya kiuchumi vya Marekani, na Muungano wa Ulaya vilivyowekewa Iran kutokana na mpango wake wa nuklia.

Thamani ya Rial ya Iran inaendelea kushuka na kuibua maswali mengi kuhusu hali ya kiuchumi na kisiasa nchini humo.

Huku jamii ya kimataifa ikiendelea kufuatilia kwa karibu mradi wa nuklia wa nchi hiyo, kwa wananchi wengi wa nchini humo swala la uchumi wao ndilo lenye umuhimu mkubwa.

Iran iliwekewa vikwazo na mataifa ya kigeni yakiongozwa na Ulaya pamoja na Marekani kufuatia wasiwasi kuwa nchi hiyo inaunda bomu la nuklia.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.