31 wauawa katika mashambulizi Allepo

Imebadilishwa: 3 Oktoba, 2012 - Saa 12:22 GMT


Takriban watu 31 wameuawa katika milipuko mitatu ya mabomu yaliyotegwa ndani ya magari katika mji wa Allepo nchini Syria

Mashambulio hayo yametokea katika eneo linalodhibitiwa na majeshi ya serikali. Mashambulio mawili yametokea katikati mwa mji na lingine nje ya ukumbi wa mji huo.

Picha za televisheni zimeonyesha uharibifu mkubwa huku majengo yakiharibiwa na pia barabara. Miili ya watu inabebwa kwa kutumia blanketi.

Mapigano kati ya majeshi ya serikali na waasi yameongezeka mjini Aleppo katika siku za hivi karibuni na kuugawa mji huo mara mbili.

Wapiganaji wa upinzani walianzisha upya mashambulizi wiki iliyopita katika jaribio la kunyakua maeneo zaidi ya mji huo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.