Serikali matatani Bangladesh

Imebadilishwa: 3 Oktoba, 2012 - Saa 14:28 GMT

Mahakama nchini Bangladesh imeitaka serikali kueleza kwa nini ilikosa kutoa ulinzi kwa waumini wa kibuddha waliolshambuliwa mnamo siku ya Jumapili.

Mahakama hiyo pia imewataka maafisa wa utawala kutoa ulinzi katika sehemu za ibada katika siku za usoni.

Mamia ya waandamanaji waliteketeza mahekalu ya kibuddha Kusini Mashariki mwa nchi na kushambulia makaazi ya watu katika kitongoji cha Cox's Bazaar.

Ghasia hizo zilisababishwa na madai kuwa picha aliyokuwa ameituma muumini mmoja wa kibuddha kwenye Facebook ilikuwa ya kuwadhihaki waisilamu. Mwanamume huyo alikana kuwahi kuichapisha picha hiyo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.