Polisi kupunguza ukali Saudia

Imebadilishwa: 3 Oktoba, 2012 - Saa 13:27 GMT

Mkuu wa kitengo cha kidini cha Polisi nchini Saudi Arabia amesema kikosi hicho kimeanzisha mfumo mpya wa maadili ya kikazi utakaopunguza ukali wa kupita kiasi wa maafisa wake uliozua tetesi miongoni mwa umma.

Sheikh Abdullatif Abdel Aziz al-Sheikh amesema sehemu ya uwezo wa kikosi hicho kinachojulikana kama Tume ya kuimarisha maadili na kuzuia madhambi, itahamishwa kwenye mashirika mengine ya Serikali.

Aidha alisema kikosi hicho cha polisi kitasitisha tabia ya kuwazuia vijana na wanaume ambao hawakuandamana na familia kuingia kwenye Vituo vya kibiashara na maduka.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.