Korea Kaskazini inajihami kijeshi

Imebadilishwa: 9 Oktoba, 2012 - Saa 15:47 GMT

Korea ya Kaskazini inasema ina makombora ya masafa marefu yenye uwezo wa kufika hadi Marekani.

Taarifa hiyo inakuja ikiwa ni siku mbili tu baada ya Korea Kusini kutangaza kuwa inaongeza uwezo wake wa mfumo wa makombora kwa eneo lote la Kaskazini, kufuatia makubaliano mapya na Marekani.

Marekani na washirika wake wamekuwa wakiishutumu Korea ya Kaskazini kujaribu kutengeneza makombora ya masafa marefu .

Taarifa iliyotangazwa kupitia televisheni ya taifa ya Korea Kaskazini imesema nchi hiyo inaimarisha uwezo wake wa kijeshi

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.