Ayatollah Khamenei akemea viongozi Iran

Imebadilishwa: 10 Oktoba, 2012 - Saa 15:02 GMT

Kiongozi wa kiroho nchini Iran, Ayatollah Ali Khamenei, amewataka maafisa wa serikali kukubali majukumu yao na kuacha kulaumiana kuhusu matatizo ya kiuchumi yanayolikumba taifa hilo.

Pia aliwakemea viongozi wa nchi za Magharibi ambao wamekuwa wakitafsiri kudodora kwa uchumi wa nchi hiyo kama athari za vikwazo vya kiuchumi ambavyo wameiwekea nchi hiyo.

Sarafu ya Iran, Rial, ilianza kushuka thamani wiki jana na kupoteza asilimia nusu ya thamani yake dhidi ya dola ya Marekani.

Wananchi wengi wa Iran, wakiwemo, washirika wake, Ayatollah Khamenei, wanalaumu Rais Ahmadinejad kwa masaibu ya kisiasa ya nchi hiyo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.