Wakimbizi wa Syria kusaidiwa Jordan

Imebadilishwa: 10 Oktoba, 2012 - Saa 13:54 GMT

Marekani imetuma washauri na watafiti wa kijeshi nchini Jordan kwa mijanajili ya kutoa usaidizi wa kibinadamu kwa wakimbizi kutoka Syria.

Katibu mkuu wa ulinzi Leon Panetta, amesema kuwa washauri hao vile vile watafanyia uchunguzi shughuli za maeneo yenye kemikali zinazotumiwa kutengeneza silaha za kivita nchini Syria.

Kwa mujibu wa afisaa mmoja mkuu wa usalama kutoka Marekani, maafisa hao wapatao 150 lengo lao kuu ni kuzuia mzozo wa Syria kusambaa hadi Jordan.

Ripoti ya umoja wa mataifa inaashiria kuwa zaidi ya wakimbizi elfu thamanini na tano wamesajiliwa nchini Jordan

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.