Shujaa wa mwisho wa uhuru Burma afariki

Imebadilishwa: 11 Oktoba, 2012 - Saa 16:03 GMT

Mmoja wa viongozi waliopigania uhuru wa Burma aliyekuwa amesalia, amefariki akiwa uhamishoni nchini China akiwa na umri wa miaka 93.

Shujaa huyo wa uhuru, Kyaw Zaw, alikuwa mmoja wa wapiganiaji wa uhuru miongoni mwa wengine thelathini waliounda jeshi huru la Burma.

Wapiganiaji uhuru wa Burma walishirikiana na wapiganaji wa Japan dhidi ya wakoloni wa Uingereza.

Kundi hilo liliongozwa na Generali Aung San,babake kiongozi wa upinzani, Aung San Suu Kyi.

Kyaw Zaw ambaye jina lake ni Shwe, aliondoka mji mkuu Rangoon kujiunga na waasi wa kikomunisti kwenye mpaka na China mwaka 1976 na kuishi katika mji wa Kusini Magharibi wa Kunming nchini China.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.