Washukiwa wa ugaidi kushtakiwa Ufaransa

Imebadilishwa: 11 Oktoba, 2012 - Saa 15:45 GMT

Serikali ya Ufaransa imesema itawafungulia mashitaka watu saba waliokamatwa mwishoni mwa wiki iliyopita wakituhumiwa kushiriki kikamilifu katika mtandao wa ugaidi.

Watu hao walikamatwa kufuatia shambulio la gruneti katika duka la mfanyabiashara wa Kiyahudi katika kitongoji kimoja cha jiji la Paris mwezi Septemba.

Jumanne, wiki hii mali ghafi ya kutengenezea bomu ilipatikana katika eneo la kuegesha magari chini ya ardhi katika mji mkuu huo wa Ufaransa.

Mwendesha mashtaka wa Ufaransa, Francois Molins amesema watu hao walikuwa sehemu ya mtandao ambao umekuwa kitisho kikubwa cha usalama cha aina yake kwa nchi hiyo tangu mapema miaka ya tisini.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.