Mdahalo wa wagombea wenza Marekani

Imebadilishwa: 12 Oktoba, 2012 - Saa 11:49 GMT

Huku zikiwa zimesalia zaidi ya wiki tatu ufanyike uchaguzi wa urais nchini Marekani , wagombea wanaowania kiti cha Makamu wa rais , Joe Biden wa Democrat na Paul Ryan, wa chama cha Republican wamekuwa na mdahalo wao wa kwanza na wa kipekee kwenye runinga juu ya kampeini .

Walikabiliana vikali katika masuala ya usalama wa taifa , kodi na huduma za afya.

Bwana Ryan amesema kuwa msimamo wa Marekani kuhusu Iran na Syria unaonyesha kuwa utawala wa Rais Obama kuhusu masuala ya nje haufai.

Bwana Biden alielezea shutuma hizo kama zisizokuwa na msingi .

Tofauti zao juu ya kodi zilitawala katika mdahalo huo . Mwandishi wa BBC mjini Washington anasema wagombea wote wawili walionekana kufanya vyema katika kuwashawishi wafuasi wao.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.