Iran yakabiliwa na vikwazo vipya

Imebadilishwa: 15 Oktoba, 2012 - Saa 12:13 GMT

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa Muungano wa Ulaya wameiwekea vikwazo vipya Iran ili kuishinikiza zaidi kuhusiana na mpango wake wa nuklia.

Wadadisi wametaja vikwazo hivyo vipya dhidi ya sekta ya benki nchini Iran kama vikali zaidi kuwahi kutolewa dhidi ya Iran.

Mawaziri pia wamekubaliana kushinikiza mazungumzo mapya kuhusu azma ya Iran kuwa na silaha za nuklia.

Kwingineko, vikwazo ilivyowekewa serikali ya Syria na Muungano wa Ulaya vimeanza pia kutelekezwa dhidi ya wafuasi wa Rais Bashar al-Assad.

Vikwazo hivyo ni pamoja na kupigwa tanji kwa mali za washirika 28 wa Asaad pamoja na makampuni mawili yenye uhusiano naye.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.