Maendeleo ya elimu duniani yadumaa

Imebadilishwa: 16 Oktoba, 2012 - Saa 15:06 GMT

Ripoti ya umoja wa mataifa inatarajiwa kuthibitisha kuwa ahadi ya jumuiya ya kimataifa kuwapatia watoto wote haki ya elimu ya msingi kufikia mwaka 2015 haitafikiwa kwa kiwango kikubwa.

Nakala ya ripoti hiyo ya UNESCO iliyoonwa na BBC inasema kuwa, baada ya kushuhudia mafanikio ya kuongezeka idadi ya watoto wanaoandikishwa katika shule za msingi katika kipindi cha miaka ya awali ya karne hii, maendeleo hayo sasa yanaonekana kurudi nyuma.

Mjumbe wa elimu ulimwenguni wa Umoja wa Mataifa Gordon Brown, amesema idadi ya watoto wasioandikishwa shule imekuwa ikiongezeka barani Afrika.

Wataalamu wa elimu wanasema kuwa wafadhili wameshindwa kutoa fedha zinazohitajika kutoa elimu kwa kila mtoto.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.