Uwindaji haramu wakithiri Afrika Kusini

Imebadilishwa: 16 Oktoba, 2012 - Saa 13:17 GMT

Afrika Kusini imesema kuwa idadi kubwa ya vifaru wameuawa kinyume na sheria mwaka huu.

Inaarifiwa vifaru mianne na hamsini wameuwa na wawindaji haramu hadi kufikia sasa.

Idadi hiyo ni kubwa kuliko vifaru kumi na tatu waliouawa mwaka 2007.

Uwindaji huo haramu unachochewa na kupanda kwa bei ya pembe za vifaru duniani ambazo hutumiwa kama dawa za kienyeji barani Asia.

Karibu nusu ya visa vyote vya uwindaji huo haramu, vimesemekana kutokea katika mbuga ya wanyama ya Kruger.

Maafisa wanasema kuwa magenge ya majambazi hutumia helikopta , miwani ya kuona kwa giza na silaha kali kuwawinda wanyama hao.

Afrika Kusini ni nyumbani kwa zaidi ya vifaru elfu ishirini ambao ni takriban asilimia tisini ya idadi yote ya vifaru barani Afrika.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.