Njama ya kuuza nguruwe kama ng'ombe

Imebadilishwa: 17 Oktoba, 2012 - Saa 10:29 GMT


Shirika la chakula nchini Sweden, limetoa onyo barani Ulaya baada ya nyama iliyouzwa kama nyama nya ng'ombe kugunduliwa kuwa nyama ya nguruwe.

Nyama hiyo inaarifiwa ilikuwa imepakwa rangi ya nyama ya ng'ombe kwa kutumia sindano.

Nyama hiyo iligunduliwa na muuza duka mmoja (Svensk Cater) bada ya mteja mmoja kurejesha nyama aliyokuwa ameinunua kutoka dukani mwake akisema kuwa ilikuwa na unyevuunyevu mwingi.

Kuna hofu kuwa nyama hiyo bandia inaweza kuwa na madhara makubwa kwa afya ya watu.

Rangi ambayo ilikuwa imepakwa nyama hiyo pia inaweza kusababisha madhara makubwa. Haijulikani ikiwa nyama hiyo ambayo ilitoka Hungary imeuzwa kwa kiwango kikubwa katika maduka na mikahawa.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.