China yalaani ziara ya Japan Yasukuni

Imebadilishwa: 18 Oktoba, 2012 - Saa 12:45 GMT

China imeshutumu vikali hatua ya wanasiasa wa Japan kuzuru madhabahu ya Yasukuni ambayo yalijengwa kwa ajili ya raia wa Japan waliouwawa wakati wa vita ikiwemo wahalifu wa kivita.

Mawaziri wawili waliungana na wabunge kuzuru madhabahu hayo siku moja baada ya kiongozi mpya wa upinzani na waziri mkuu wa zamani Shinzo Abe kutoa heshima zake .

Shirika la habari la serikali ya uchina Xinhua liliitaja ziara hiyo kama kitendo cha madharau.

Uhasama kati ya mataifa hayo umekuwa ukiendelea kuhusiana na visiwa katika ziwa la East China.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.