Wapiganaji wa Al Qaeda wauawa Yemen

Imebadilishwa: 18 Oktoba, 2012 - Saa 12:22 GMT

Maafisa wa usalama nchini yemen wamesema kuwa takriban wapiganaji saba wa kundi la kigaidi la Al Qaeeda wameuwawa katika mashambulio yaliyotekelezwa na ndege za Marekani zisizo-kuwa na rubani.

Wanasema makombora kutoka kwa ndege hizo yalirushwa kwa shamba moja karibu na mji wa kusini wa Jaar, kufuatia taarifa kuwa wapiganaji walikuwa wanapanga kuvamia mji huo.

Mji wa Jaar ni miongoni mwa miji miwili ambayo ilikuwa ngome ya Al qaeeda Kusini mwa nchi hiyo.

Ilitwaliwa na Kundi la Al qaeeda wakati wa mapinduzi dhidi ya Rais wa zamani Ali Abudullah Saleh mwaka jana lakini jeshi la serikali ya Yemen ikaiteka tena mnamo Juni mwaka huu.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.