Wagiriki waandamana kupinga serikali

Imebadilishwa: 18 Oktoba, 2012 - Saa 13:00 GMT

Maelfu ya raia wameandamana katika mji mkuu wa Ugiriki, Athens kupinga hatua nyengine ya serikali kupunguza matumizi ya pesa za umma.

Vyama vya wafanyikazi nchini humo vimeapa kutatiza shughuli nchini humo kwa masaa ishirini na manne huku wahudumu wa taxi, wafanyikazi wa feri na waelekezaji wa ndege wakisitisha huduma zao.

Maandamano hayo yanafanyika huku waziri mkuu wa Ugiriki Antonis Samaras akijiandaa kukutana na viongozi wengine wa bara Ulaya kujadili namna ya kukabiliana na mzozo wa kiuchumi.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.