Boko Haram washambulia kwa mabomu

Imebadilishwa: 19 Oktoba, 2012 - Saa 16:11 GMT

Wapiganaji wa Boko Haram nchini Nigeria, wamefanya mashambulizi ya mabomu katika mji wa Kaskazini Mashariki wa Potiskum na kisha kufyatuliana risasi na polisi.

Watu kadhaa waliuawa katika makabiliano hayo na polisi.

Baadhi ya majengo yaliyoshambuliwa ni shule, majengo ya serikali na vituo vya polisi.

Maafisa wa usalama, walisema kuwa vurugu lilifanyika Alhamisi usiku lakini bado kulikuwa na mabomu ambayo hayakulipuka mjini humo.

Kundi la wapiganaji wa Boko Haram ambalo limekuwa likiendesha harakati zake Kaskazini mwa Nigeria, limelaumiwa kwa mashambulizi hayo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.