Mwanajeshi aliyempiga risasi rais ajieleza

Imebadilishwa: 22 Oktoba, 2012 - Saa 14:25 GMT

Mwanajeshi aliyempiga risasi kwa bahati mbaya Rais wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz mapema mwezi jana amesimulia matukio ya siku hiyo katika televisheni ya taifa.

Rais huyo anaendelea kupokea matibabu nchini Ufaransa.

Luteni Elhaj Ould H'Moudy alisema alikuwa amevalia nguo za kiraia alipojaribu kuzuia magari ya watu wasiojulikana katika kuzuizi cha polisi viungani mwa mji mkuu Nouakchott.

Alisema kuwa magari hayo yalikimbia kwa kasi ndipo akalazimika kufyatua risasi bila kujua kuwa Rais alikuwa ndani ya gari hilo.

Aidha alsema jeshi limemuondolea lawama zozote.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.